Kutoka nafsini mwangu
MSTARI UKO WAPI
Materialism ni neno la lugha ya kiingereza limaanishalo ile hali ya kufikiri kuwa mali nyingi tu ndizo zinazo weza kumpatia mtu utoshelevu na kutojali mambo mengine kama ya kiroho na kitaaluma.
Sijui kama ni mimi tu, ila nadhani hata wenzangu wengi wanapitia hali hiyo hakuna kipindi uliwahi kuridhika na mali au pesa unayoipata kama ni katika biashara au mshahara.
Unapopata mali au pesa, hapo hapo ndipo tamaa yakupata nyingine nyingi zaidi huwa inakuja, kwa kadri unaposogelea malengo yako basi hujikuta tayari ulisha weka malengo mengine njiani na yako mbali sana kuyafikia.
Kuna dhana mbali mbali, kuna ile inayosema jiwekee malengo hadi utakapo yaangalia malengo yako utetemeke, kuna ile nyingine inasema unaweza fikia popote hata anga(sky) haliwezi kuwa kizuizi. Swali linabakia je unafikiaje hapo?? Je katika kufikia malengo yako haushushi viwango vya taaluma yako, ukristo wako au mtizamo wako wowote ule wa ndani.
Sina ubishi hata kidogo, ila kwa mawazo yangu, kutoka katika nia (mind) yangu kwa vile tunavyo tamani sana kufikia malengo yetu kuna haja kubwa ya kuangalia mikakati yetu, matokeo ya karibu na matokeo ya muda mrefu.
Wengi wetu tumechanganya sana tunawasifu wenye mali na pesa nyingi hata katika nyumba za ibada tunawaita walio barikiwa.
Mwisho: Maisha ni zaidi ya pesa na mali ni vizuri zaidi kuangalia vitu ambavyo kweli ni kiini cha uwepo wetu duniani wakati tukitafuta mali na pesa kutusaidia kufikia kile kiini. Kama kweli ni mwana taaluma basi taaluma yako isipindishwe na jitiada mbali mbali za kutafuta mali au pesa na vile vile kwa wa kristo basi ni vizuri kuangali kiini kikubwa cha maisha yetu ya duniani kile ambacho tuko tayari kufa kwaajili yake ambacho ni uzima wa milele.
No comments:
Post a Comment